Jenista Mhagama, Waziri wa Afya.
Hayo yamesemwa na Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbe, Dokta Clara Mwansasu, akiongea na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, baada ya kumaliza kikao kazi na mke wa mtoto wa Mfalme kutoka Uingereza na akielezea changamoto zilizopo.
"Tumeweza kuwakinga wananchi wengi ili wasipate ulemavu wa kudumu na Serikali imeweka afua mbalimbali za magonjwa tiba, elimu kwa jamii ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata uelewa juu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele, kwa mwaka 2024 tumewekeza kuwafikia wananchi wengi zaidi na mpaka sasa tumefikia halmshuri 60, wagonjwa wa trakoma 167, 000 wamefanyiwa upasuaji, wagonjwa milioni 10,440,000 wapo hatarini kupata ulemavu wa kudumu", alisema Dkt. Clara Mwansasu, Meneja mpango NTD's
"Changamoto ya fedha imekuwa kubwa, Serikali inafanya effort kuhakikisha fedha inapatikana na tukipata fedha tutafikia watu wengi zaidi, changamoto nyingine ni Wahudumu wa afya, Mila na desturi kuna watu wanakataa huduma , tuongeze uelewa kuwa ugonjwa wa trakoma unatibika mtu akifanyiwa upasuaji atapona na atarudi kwenye hali yake ya kawaida", alisema Godwin Kabalika, Mkurugenzi wa shirika la sightsavers.
Leo mapema mke wa mtoto wa Mfalme, Sophie Helen, alifanya ziara katika kituo cha Afya magomeni kwa lengo la kuona jitihada za misaada inayotolewa na Serikali ua Uingereza ambapo aliambatana na Balozi wa Uingereza ambaye anaelezea ziara hiyo.
"Atakuwa na ziara kwa wiki hii yote leo tumetembelea miradi inayodhaminiwa na Serikali ya Uingereza lakini, lakini kesho ataenda Pwani kisha ataenda Arusha pamoja na Zanzibarm, kikubwa anakuja kuangalia zile fedha zinazotolewa utekelezaji wake, lakini pia kuangalia namna wanavyoweza kupunguza changamoto ya Watanzania kupata ulemavu wa kudumu", alisema Mariane Young, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Jenista Mhagama, anaelezea mikakati ya Serikali kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
"Shirika la Afya Duniani linataka mpaka 2030 tuwe tuekwisha kupambana na magonjwa hayo yote na yameondoka katika nchi zetu, na sisi kwakweli tumejipanga mpaka 2027 at least tuwe tumevuka asilimia 95 na tuwe tunaelekea kuyatokomeza, na kuongeza eneo la tathmini na ufatiliaji na hilo nalo ni eneo tunatumia kujipima", alisema Jenista Mhagama, Waziri wa Afya.