Thursday , 12th Sep , 2024

Uongozi wa Yanga SC umeitaka kamati ya sharia na hadhi ya wachezaji ya shirikisho la soka nchi TFF kumtangaza mchezaji Yusuph Kagoma kuwa mchezaji halali wa Yanga SC lakini pia wachukua hatua za kikanuni kwa kufanya makosa ya kusaini mikataba na vilabu viwili kwa wa kati mmoja.

Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu Yanga Simon Patrick amewasilisha msimamo wa klabu hiyo kwenye sakata la mgogoro wa kimkataba baina ya mchezaji Yusuph Kagoma na Yanga. Yanga ikiwa inaamini mchezaji huyo ni

"Tarehe nne mwezi wa tatu mwaka huu Uongozi wa Klabu ya Yanga ulianza kufanya mazungumzo na Uongozi wa Fountain Gate FC kwa ajili ya kutaka kumnunua Kagoma  pande zote mbili zilifikia muafaka na Fountain Gate  iliitaka Yanga iwalipe milioni 30 kwa awamu mbili ili iweze kumchukua  ambazo walitaka walipwe milioni 15 mwezi wa nne na milioni 15 wazilipe mwezi wa sita, amesema  Patrick.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo ameweka wazi kuwa Aprili 30 mwaka huu Uongozi wa Yanga uliulipa Uongozi wa Klabu ya Fountain Gate FC.