Friday , 23rd Aug , 2024

Timu ya Yanga SC imetamba kwenda kupata ushindi kwenye mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa barani Afrika 2024-25 dhidi ya Vital'O ya Burundi utaopigwa jumamosi ya Agosti 24, 2024 katika uwanja wa Azam Complex , Chamazi Saa 1 Usiku Jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkufunzi wa Yanga SC  Miguel Gamondi amesema wanajiamini na matokeo waliyoyapata kwenye mchezo uliyopita lakini bado wanaziheshimu dakika 90 za mchezo wa kesho huku lengo lao kubwa ni kufuzu kwenda hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

'' Siwezi kusema kuwa hatuwezi kufungwa goli tano, lakini sio jambo ambalo natarajia kuliona likitokea. Nina matumaini makubwa sana na wachezaji. Nafahamu watakuja kwa nguvu kutafuta magoli nasi tumejiandaa kwa kila mbinu" Miguel Gamondi - kocha Mkuu Yanga.

Aidha wapinzani wa Yanga SC,Klabu ya Vital’O ya Burundi kupitia kwa benchi la ufunfi la klabu hiyo wametamba kwenda kufanya vyema kwenye mchezo wa kesho na kuvuka kwenda hatua inayofuata licha ya kuwa na mzigo mkubwa wa magoli 4-0 waliyofungwa kjwenye mchezo wa awali walipocheza na Yanga mnamo Agosti 17-2024.

Yanga SC ikivuka hatua ya kwanza itapambana na mshindi baina ya CBE ya Ethiopia au SC Villa ya Uganda ambapo kwenye mchezo wa kwanza Villa alikubali kichapo cha magoli 2-1 kwenye dimba la Taifa la Mandela mjini Namboole nchini Uganda