Wednesday , 21st Aug , 2024

Uongozi wa timu ya JKT Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania Bara umesema malengo yao msimu huu wa mashindano 2024-25 ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu na kupata uwakilishi kwemye michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu ujao.

Afisa habari wa timu JKT Tanzania Masau Bwire ameiambia EATV Habari kuwa msimu huu wamejipanga na  wapo vizuri kila idara hivyo hakuna sababu ambayo itawakwamishwa wao kutochukua ubingwa wa Ligi kuu na kuandika historia.

''Kuchukua ubingwa wa soka la nchini hii na tumejiweka vizuri kwa kuboresha hivyo tuwaambie timu zingine kichapo cha kizalendo hakiepukiki kwasababu tumejipanga''amesema Bwire.

Kwa upande mwingine Bwire ameweka wazi mabadiliko waliyofanya kwenye uwanja wao wa nyumabani wa Meja Jenerali Isamuhyo watakaotumia kwenye michezo ya mashindano msimu huu. Huko moja ya eneo lililofanyiwa maboresha ni sehemu ya majukwaa ambayo awali hayakuwepo.

Kikosi cha JKT Tanzania Kitashuka dimbani agosti 28 kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu msimu mpya wa 2024-25 dhidi ya Azam FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo , Mbweni , jijini Dar es salaam .