Tuesday , 13th Aug , 2024

Jeshi la Polisi nchini limesema licha ya kuachiwa huru kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA, waliokuwa wanajiandaa kufanya kongamano la kuadhimisha siku ya vijana duniani Jijini Mbeya, litaendelea kuimarisha ulinzi wa maeneo mengine nchini kuhakikisha wanazuia wenye fikra za

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi La Polisi CP Awadhi Juma Haji

kuendelea na kongamano hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi La Polisi CP Awadhi Juma Haji wakati akizungumzia hatua ya kuachiwa huru kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA na viongozi wao ambao walifika mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya kongamano la kuadhimisha siku ya vijana duniani ambalo lilipigwa marufuku na jesni la polisi kwa kile kilichoelezwa kuwa lina viashiria vya uvunjifu wa amani.
 
Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa ni Fereeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti, Tundu Antipas Lissu, Katibu Mkuu wa, John Mnyika, viongozi na wanachama wengine wa chama chadema ambao idadi yao inafikia 520 walikamatwa na polisi katika maeneo mbalimbali nchini wakituhumiwa kutaka kufanya kongamano lililopigwa marufuku.