Sunday , 11th Aug , 2024

Msanii wa Bongofleva Mandojo amefariki dunia leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Picha ya Mandojo enzi za uhai wake

Msanii mwenzake aliyefanya naye kazi kwa ukaribu Domokaya na Soggdoggyanter wamethibitisha taarifa hiyo ya kifo cha Mandojo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu mmoja ambaye alimuitia mwizi.