Wednesday , 7th Aug , 2024

 Rais wa 45 na Bilionea kutokea nchini Marekani, Donald Trump ametangaza kufanya mahojiano na Bilionea na mmiliki wa mtandao wa ''X'' Bw. Elon Musk jumatatu ya wiki ijayo yaani Tarehe 12 Agosti.

Kupitia mtandao wa kijamii ambao anaumiliki yeye mwenyewe ''Truth social'' Trump aliandika ''Jumatatu nitafanya mahojiano na Elon Musk''

Bado haijafahamika mahojiano hayo yataruka kwenye mtandao wake ambao unafahamika kama ''Truth social'' au kupitia mtandao wa Bilionea Elon Musk, Twitter zamani ''X'' kwa sasa.