Thursday , 25th Jul , 2024

Baada ya kufanya ukaribisho wa mchezaji Kilian Mbappe, mbele ya mashabiki zaidi ya elfu 80 kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu, klabu ya Real Madrid inakuja tena kwenye vichwa vya habari.

 
Kupitia wavuti rasmi wa klabu hiyo, taarifa kubwa ni hii ya kuvunja historia kwa kuwa klabu ya kwanza duniani kufikia mapato ya dollar Bilioni '1.73' ambayo ni zaidi ya Trilioni '2' kwa shilingi ya ki-Tanzania.

Mapato haya ni sawa na ongezeko la asilimia 27 toka msimu uliyopita, na ongezeko hili halijajumuisha mapato yaliyopatikana kutokana na uhamisho wa wachezaji.