
Amesema msimu uliopita hawakufanya vizuri sana kwenye safu hiyo na kushindwa kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa na kuishia kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
-
Simba msimu uliopita wa 2023/24 walifunga jumla ya mabao 59 na kufungwa 25 tofauti na 2022/23 ambao walifunga mabao 75 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 17, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
-
Kazi kubwa ambayo anaifanya Kocha Fadlu ni kuwapa mbinu washambuliaji wakiongozwa na Kibu Denis, Freddy Michael, Steven Mukwala na Joshua Mutale mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.
-
Matola ameiambia EATV kuwa kocha Fadlu anapita katika njia ya Simba ambao makocha waliofanikiwa kipindi cha timu hiyo ilipofanikiwa na tangu amekabidhiwa anasisitiza zaidi washambuliaji kuwa makini wanapokuwa uwanjani.