Kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wamesema ulianza kuwaka majira ya saa 10 usiku wa kuamkia leo ambapo umeteketeza mali zilizokuwemo.
Miongoni mwa wageni waliokuwa kwenye nyumba hiyo amesema kuwa alikuwa amelala akaanza kusumbuliwa na moshi mkali huku akisikia kelele za wenzake wakiomba msaada na yeye akaamka na kuanza kutafuta njia ya kutoka.