Friday , 19th Jul , 2024

Miili ya wanafunzi wawili wa shule ya msingi Mahaha iliyopo kata ya Bunamhala halmashauri ya mji wa Bariadi ambao walikufa maji wakati wakiogelea kwenye dimbwi lililochimbwa kwaajili molamu ya kujengea barabara, imezikwa leo mji Bariadi.

Ni katika ibada ya kuombea miili ya wanafunzi wawili wa darasa la saba waliofahamika kwa majina ya Anna Mayunga umri miaka 14 na Martha Dickson umri miaka 13 ambao walipoteza maisha wakati wakiogelea kwenye dibwi.

Ni kijana aliyeingia ndani ya dimbwi hilo kutoa miili ya wanafunzi hao hapa anazungumzia namna alivyopata taarifa.
“hili tukio lilinikuta nikiwa nyumbani nilipigiwa simu na watu kwenda kuokoa wale wanafunzi nilipofika pale nikakuta kuna watu wengi wamejaa pale kwa vile mimi najua kuogelea niliingia kule na kuzama nikamtoa huyu mmoja wapo ambaye ni Anna Mayunga watu walikuwa wamejaa tukajaribu kuokoa maisha yao tukawapeleka hospitali tulipofika hospitali madaktari wakapima wakakuta watu walishafariki” LUHINDA GISADU,Aliyetoa miili kwenye dimbwi.

Maombi ya ndugu pamoja na kijana aliyetoa miili kwenye maji ni kufukiwa kwa madimbwi yote au yawekewe uzio ukienda sambamba na tangazo la hatari.

"Na tunashukuru mkuu wa wilaya kufika kwenye tukio akaja tunaomba awafatilie wale wa tarura liweze kufukiwa maana linaleta majanga katika mtaa wetu"- LUHINDA GISADU,Aliyetoa miili kwenye dimbwi.

"Hawa wakandarasi wanapokuwa wanamaliza basi wayafukie kwasababu yatatuondoa sana mifugo,watoto wananchi kwa ujumla na kama hawawezi basi kufukiwa yawekewe uzio ambao mtu atashindwa kupita pale akifika anajua kuna hatari na kuweka vibao ambavyo vinaonesha hatariâ", JONH MAFURU,Babu wa marehemu.

Diwani wa kata ya Bunamhala anasema si tukio la kwanza watu kufa maji kwenye madimbwi,wakati huo huo akitoa salamu za serikali afisa elimu msingi wa halmashauri ya mji wa Bariadi amesema msiba yote miwili umegharamiwa na serikali.

"Sawa miundombinu tunafulahi wanapokuwa wanatutengenezea lakini sasa serikali iwaagize wanapokuwa wanachimba haya mashimo baada ya kuwa wamechukua molamu either wayafukie au watengeneze uzio na kuweka alama za hatari kwa maana kwamba watu wasifike maeneo hayo kwani tumekuwa na misiba mingi ambayo inasababishwa na haya mashimo wamama wengi wanakufa kwaajili ya haya mashimoâ"NKAMBA ZABLON,Diwani kata ya Bunamhala.

"Tumeweza kugharamia majeneza yote mawili huduma kwa waombolezaji chakula lakini pia kwaajili ya maji ni wajibu wetu kama halmashauri ya mji wa Bariadi kwa kushirikiana na walimu lakini pia jamii iliyozunguka shule kuona aja kubwa na sababu ya kuwalinda watoto wetu na kwa uangalifu wa hali ya juu", PALTHA CLEOPHACE,Afisa elimu msingi halmashauri ya mji Bariadi.