Friday , 19th Jul , 2024

Rais William Ruto ametangaza mawaziri kumi na moja kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri. Katika hotuba yake kwa taifa , rais Ruto amesema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa wiki ijayo baada ya mashauriano.

Rais amesema kwamba uteuzi huo ambao ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali - unafuatia mashauriano katika sekta ya kisiasa katika jaribio la kurudisha amani na utulivu nchini.

Orodha hiyo pia ilikuwa na Mawaziri sita waliofukuzwa kazi, ambao sasa wanarejea katika wizara tofauti, huku Prof. Kithure Kindiki, Alice Wahome na Adan Duale wakiendelea kushikilia nafasi zao za zamani.

Mawaziri walioteuliwa ni:

Kithure Kindiki - Waziri wa masuala ya Ndani

Dkt. Debra Mulongo Barasa - Waziri wa Afya

Alice Wahome - Waziri wa Ardhi

Aden Duale - Waziri wa Ulinzi

Davis Chirchir - Waziri wa Uchukuzi

Rebecca Miano - Mwanasheria Mkuu

Soipan Tuya - Waziri wa Mazingira

Julius Migosi - Waziri wa Elimu

Eric Muriithi - Waziri wa Maji

Dr Margaret Ndungu- Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia

Andrew Karanja - Waziri wa Kilimo