Thursday , 18th Jul , 2024

Kenya imepoteza takribani shilingi Bilioni 6 kutokana na maandano yaliyofanyika na vijana maarufu kwa jina la Gen Z nchini humo na hasara hiyo imetokana na vurugu zilizofanyika na maandamano

kiwahutubia wanahabari leo, Mwaura amesema taifa hili limepata madhara mengi kutokana na maandamano ya vijana wa Gen z , akisema nchi hii imepata hasara ya shilingi bilioni 6 kutokana maandamano hayo . Mwaura amesema kuna hofu kwamba ikiwa maandmano hayo yataendelea, uchumi wa nchi hii utaathirika vibaya .

Mwaura ameeleza kuwa nchi ilipoteza mabilioni kutokana na kufungwa kwa biashara wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumanne na Alhamisi tangu Juni 18, 2024.

Ameongeza kuwa biashara kadhaa pia ziliporwa na mali kuharibiwa na wahuni waliojipenyeza katika maandamano hayo ya amani na kusababisha fujo na ametoa wito kwa vijana kusitisha maandamano na kutoa nafasi ya mazungumzo na serikali.

Kulingana naye, Rais William Ruto ameonyesha nia njema kwa kuachilia matakwa kadhaa ambayo ni pamoja na kufuta baraza lake la mawaziri, kufuta mashirika 47 ya serikali, kusimamisha uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Tawala, kukataa Mswada wa Fedha wa 2024 miongoni mwa mengine.

Vijana bado wanapanga kuendeleza maandamano kupinga ubadhirifu unaoonyeshwa na viongozi wa serikali, uwajibikaji na utawala bora.
Pia wamemtaka rais kujiuzulu wadhifa wake