Mkurugenzi wa Michezo kwa soka la Wanawake Brighton & Hove Albion Zoe Johson amesema tunafuraha ya kumkaribisha Aisha ndani ya Brighton, Amekuwa na msimu mzuri na mwenye muendelezo mkubwa akiwa Sweden akiiwakilisha Hacken kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya 2023-24”.
Aisha Masaka mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Hacken mnamo mwaka 2022 akitokea klabu ya Yanga ambapo kabla ya hapo aliwahi kuichezea timu ya Alliance FC Mwanza huku mpaka sasa ameichezea timu ya Tanzania “Twiga Stars ” kwenye michezo 15 tangu mwaka 2021