Kajula aliingia Simba mnamo Januari 2023 na kusaini kandarasi ya miezi 6 uliokuwa na kipengele cha kuongeza muda huku alirithi mikoba ya Barbara Gonzalez aliyeondoka ndani ya Simba SC kipindi hicho.
Kajula anaondoka ndani ya Simba SC akishinda kombe la Muungano 2024 pamoja na Ngao ya Jamii msimu 2023-24,kufika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika 2023-24 pamoja na kuanzisha mifumo bora ya Wanachama kama Simba Executive Network kwa ajili ya kuiongezea mapato ndani ya klabu hiyo.
Utamkumbuka kwa lipi Imani Kajula ndani ya Simba SC?