Sunday , 14th Jul , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga linamshikilia kada wa CHADEMA, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Kada wa CHADEMA

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 14, 2024, na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Zacharia Bernard, ikiwa zimepita siku 29 tangu kada huyo adaiwe kupotea.

Akizungumza Kamanda Benard, amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.