Sunday , 23rd Jun , 2024

Rais wa Kenya William Ruto amewapongeza vijana walioandamana kwa amani nchini humo kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2024/2025 na kusema kwamba walifanya jukumu la kidemokrasia na yuko tayari kukaa na kuzungumza nao na lengo kuu likiwa ni kujenga Taifa moja.

Rais wa Kenya William Ruto

Rais Ruto ametoa kauli hiyo leo Juni 23, 2024, wakati wa ibada ya Jumapili

"Nawapongeza vijana kwa kujitokeza na kushughulika na mambo ya Taifa lenu la Kenya, Tutakuwa na mazungumzo ya pamoja na kuchanganua changamoto zenu na tutafanya kazi kama Taifa," amesema Rais Ruto