Friday , 21st Jun , 2024

Mbunge wa Jimbo la Maswa ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Stanislaus Haroon Nyongo  amewataka viongozi wa dini nchini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan 

Stanislaus Haroon Nyongo  ametoa kauli hiyo baada ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa Katoliki Parokia ya Nyalikungu mjini Maswa kwa kutoa mifuko ya saruji ambayo imekabidhiwa kupitia kwa Katibu wake wa jimbo Marco Bukwimba. 

Akizungumza  na uongozi wa Kanisa hilo, Bw. Bukwimba amesema mifuko hiyo ya awali, ni sehemu ya mchango wa mifuko 100 aliyoahidi kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo. 

"Mhe Nyongo kama alivyokuwa ameahidi ataendelea kuchangia ujenzi wa kanisa bila kuchoka, kama vile kanisa linavyoliombea amani Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake, bila kuchoka." 

Akizungumza kwa niaba ya kanisa hilo Padre wa Parokia hiyo Bw. Deogratias Ntindigo amemshukuru Mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itasaidia katika ujenzi wa Kanisa hilo.