Wednesday , 5th Jun , 2024

Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa baada ya Lori aina ya Scania yenye namba za usajilii T 979 CVV lililokuwa limebeba kokoto kufeli breki na kugonga gari aina ya coster lenye namba T 167 DLF lililokuwa na abiria, haria, pikipiki na guta lililobeba mahindi. 

Baadhi ya Askari wakiwa eneo la Ajali kwaajili ya Uokoaji

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa scani yenye namba T979CVV/T758 BEU kushindwa kulimudu gari hilo kwenye kwenye mteremko na kwamba tayari Jeshi la Polisi linamshikilia dereva huyo ambaye anaendelea na matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi na milli ya marehemu imepelekwa Hospitalini hapo kwa hifadhi na kusubiri k utambuliwa.