Friday , 31st May , 2024

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo, amepata Ubalozi wa kutoa elimu kuhusu changamoto ya afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Jijini Dodoma ambapo majukumu yake yatakuwa ni pamoja na kusaidia kufikisha elimu ya ufahamu kuhusu tatizo la afya ya akili.

hususani kwa vijana.

Ubalozi huo amepata baada ya kupata mwaliko wa kutembelea hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amepata elimu kuhusu tatizo la afya ya akili linavyowakabili watumishi wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalimbali, wapambanaji wengine kwenye majukumu yao ya utafutaji, vijana na wanawake baada ya kujifungua.