Tuesday , 7th May , 2024

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi, ameiomba serikali kwamba ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner inayotarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwezi huu wa Mei ipewe jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kumpa heshima yake anayostahili.

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

Kauli hiyo ameitoa bungeni jijini Dodoma wakati akichangia kwenye makadirio ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi

"Mwaka huu ni wa 25 toka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipofariki dunia ingawa amegoma kufa, mimi napendekeza ndege yetu kubwa ya Dreamliner ambayo haijaja tuipe jina la Julius Nyerere Kazi Iendelee kwa kuuenzi Muungano wa miaka 60 na kumpa heshima Baba wa Taifa ambaye miaka 25 iliyopita Mwenyezi Mungu alimchukua lakini bado yu hai na kufanya hivyo sisi hatutakuwa wa kwanza, Shirika la Ndege la Afrika Kusini ndege yao kubwa kuliko zote ya Airbus mwaka 2003 Mandela alipofikisha miaka 85 waliipa jina lake," amesema Profesa Kabudi