
Uvuvi
Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha amekiri kuwepo kwa tatizo hilo nchini na kuahidi kulitokomeza kwa kuboresha sekta ya uvuvi nchini ili ilete tija kwa taifa.
Naibu Waziri Ole Nasha amesema mpaka sasa wameanzisha vituo 25 vya doria katika maziwa makubwa, mwambao wa bahari pamoja na mipaka ya nchi ili kufanya ukaguzi kwenye maduka ya zana za uvuvi ili kubaini ubora wa zana hizo.
Aidha wameanzisha vikundi vya usimamizi wa rasimali za uvuvi 754 vilivyoanzishwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuishirika jamii moja kwa moja juu ya kutambua athari za uvuvi haramu kwa maendeleo ya nchi.