Tuesday , 30th Apr , 2024

Moja ya story kubwa kule Marekani ni kubuma kwa show ya rapa wa Migos Quavo ukumbi wa Hartford Healthcare Ampitheater, Connecticut Marekani wikiendi hii.

Picha ya Quavo

Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua mashabiki 5700 lakini waliojiotokeza kushuhudia show hiyo ya Quavo walikuwa watu zaidi ya 100 tu.

Taarifa hiyo imeibua muendelezo wa bifu zito linaloendelea kati ya Quavo na Chris Brown, ambapo inasemekana Chris Brown amenunua tiketi za show hiyo ili kumfelisha Quavo.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea kwa 50 Cent kununua tiketi za mbele kwenye show ya Ja Rule na kukaa peke yake ili kuonekana show hiyo haikuingiza watu.