![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/04/17/kichanga.jpg?itok=PEXmPoUw×tamp=1713374894)
Mikiness Chisunga akiwa kwenye maumivu makali baada ya kufiwa na kichanga wake
Akiwa nyumbani kwake mwanamke huyo ameshindwa kuelezea tukio hilo baada kudai anakabiliwa na maumivu makali yanayotokana na kukosa huduma yoyote ya kimatibabu
Baba wa familia hiyo Bw. Enock Kaminyoge amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati akifanya jitihada za kumpeleka mke wake katika Zahanati ya kijiji jirani.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Shida Mwampashi amesema kuwa wananchi wanaokadiriwa kufikia 800 wakiwemo wa vijiji jirani wanakosa huduma za afya kwa sasa kutokana na Zahanati kufungwa kwa kukosa muhudumu.
EATV inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ili kuelezea utatuzi wa changamoto hiyo.