![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/04/15/mtumishi.jpg?itok=z43lxS_7×tamp=1713192493)
Askofu Mar Mari Emmanuel
Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari mshukiwa amekamatwa baada ya kufanya tukio hilo la kumjeruhi askofu Mar Mari Emmanuel ambaye kwa mujibu wa taarifa ya polisi hakupata majeraha makubwa ya kuhatarisha uhai wake.
Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha mtu aliyevaa mavazi meusi akimsogelea askofu huyo na kuanza kumshambulia wakati akitoa mahubiri.