![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/04/12/Untitled-1.jpg?itok=wJr0IbNT×tamp=1712950326)
Ukuta wa nyumba ambao umebomoka na kuua mtoto
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema baada ya mvua kunyesha walisikia kishindo cha ukuta ukidondoka na baada ya kufika chumba cha watoto wakakuta ukuta umewafunika watoto wake na baada ya jitihada za kuwaokoa mmoja alikuwa mefariki dunia na mwingine akiwa na hali mbaya.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani ambaye amesema kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo, wananchi wanaoishi maeneo ya maporomoko ya maji wanapaswa kuhama ili kuepuka madhara zaidi.