Wafanyabiashara
Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao wanadai hawakupewa elimu kuhusu kodi hiyo ya huduma (Service levy) huku wakilalamikia kudaiwa kwa nguvu.
Aidha, wamesema hawatakuwa tayari kufungua biashara zao iwapo hawatasikilizwa na kufanyiwa kazi malalamiko yao.
"Tatizo kubwa ni tozo ambazo tumekuwa tukiletewa pasipokuwa na elimu yoyote, zipo juu ya uwezo wa mfanyabiashara na wanadai kwa nguvu, kwahiyo tumeamua kugoma kwa muda usiojulikana hadi watusikilize," amesema mmoja wa wafanyabiashara hao.
Pamoja na uongozi wa wilaya hiyo akiwemo Katibu tawala na Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mwanza kufika kwa nyakati tofauti kuwataka wafungue biashara bado wameendelea na msimamo wao.