Jambo lenyewe ni kuruhusu upakuaji wa Apps kutokea vyanzo vingine, Unapozungumzia vyanzo vingine ni kwa maana ya nje ya masoko maalumu ya upakuaji Apps ambayo yanafahamika mfano AppStore kwa watumiaji wa iPhone na Playstore kwa watumiaji wa Android.
Mbali na masoko hayo watumiaji wa iPhone kwa sasa ambao watawezesha IOS 17.4 kwenye vifaa vyao watafanikiwa kupakua GB-WhatsApp na Apps nyinginezo ambazo hazimo kwenye masoko husika.
NB: Matumizi ya Apps ambazo hazitoki kwenye masoko husika ni hatari kwa usalama wa simu na mtumiaji, hivyo ni vyema ukajihadhari. Na vile vile maboresho ya upakuaji wa GB WhatsApp na Apps nyinginezo yatawahusu watumiaji wa iPhone walio kwenye nchi zilizopo umoja Ulaya (EU) tu kwa sasa.