Simba iliingia kwenye mchezo huo ikitokea kuichapa Jwaneng Galaxy 6-0 kwenye mchezo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi iliyopita, lakini huko Jamhurii, mabao mawili ya Samson Mbangula yalitosha kuwalaza na kupoteza mechi ya pili kwenye ligi hiyo msimu huu.
Mbangula alifunga katika kila kipindi, huku Simba ikipata bao la kujifariji kupitia kwa kiungo wake wa kati, Fabrice Ngoma dakika 89. Na sasa, Mbangula amefikisha mabao saba katika ligi hiyo, huku timu yake ya Prisons ikivuna pointi 27 katika mechi 19, ikishika nafasi ya tano katika msimamo. Simba imebaki kwenye nafasi ya tatu na pointi zao 36 ilizovuna kwenye mechi 16.