Monday , 4th Mar , 2024

Nchi ya  Somalia imeingia katika Jumuiya ya Afrika mashariki na kufanya mtangamano huo kuwa na nchi wanachama nane.

Waziri anaeshughulikia masuala ya viwanda na bishara nchini somalia Jibril Abdirashid Haji pamoja na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Peter Mathuki wakishika endera ak bendera kiashirio cha kuingia katika umoja wa jumuiya hiyo katika makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Arusha.

Haya yanajiri baada ya nchi ya Somalia kuwasilisha nyaraka za kukubali itifaki za Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika Makao Makuu yake  jijini Arusha. 

Sekretarieti ya EAC siku ya Jumatatu ilichapisha kwenye mtandao wa Twitter kwamba Somalia imepata uanachama kamili "baada ya kuweka Hati yake ya UTHIBITISHO  na Katibu Mkuu" wa Jumuiya hiyo.

Novemba mwaka jana, Wakuu wa Nchi wanachama wa EAC walikubaliana kuiingiza Somalia katika umoja huo hatua ambayo inalenga kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini humo, ambao bado unaimarika kutokana na miongo mitatu ya vita.

Somalia inakuwa mwanachama wa nane wa EAC baada ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.