Friday , 1st Mar , 2024

Waziri ya Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu amevielekeza vituo vyote vya afya binafsi na vya umma vilivyoingia Mkataba na NHIF kuendelea kutoa huduma kulingana na Mikataba yao waliyoingia huku akiwataka Waganga Wakuu wa Mikoa kusimamia maelekezo ya Serikali. 

Waziri ya Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa vituo vyote vya afya binafsi na vya umma vilivyoingia Mkataba na NHIF kuendelea kutoa huduma.

Akiwa Mkoani Lindi leo Machi 01, 2024 Waziri Ummy ameyasema kila mtoa huduma za afya kwa wanachama wa NHIF ameingia mkataba na NHIF hivyo lazima wazingatie masharti ya mikataba walioingia na NHIF katika kuwahudumia wanachama wake. 

"Napenda kutoa rai kwa hospitali zote binafsi zilizositisha kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF ziendelee kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF"

"Kamati ya Kitaalam niliyoiunda iendelee kufanya majadiliano na watoa huduma wakati huduma zikiendelea kutolewa, nasisitiza majadiliano yataendelea wakati huduma zinaendelea kutolewa" amsisitiza Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha Waziri Ummy amezelekeza hospitali na vituo vyote binafsi na vya umma kuendelea kuwapokea wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwani hili ni takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo  binafsi vya afya na kanuni yake namba 32, na kwamba kutokuwapokea wagonjwa wa dharura ni kuvunja sheria.

"Hatutamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye  atakiuka sheria ya kutoa huduma hivyo naomba wabadilishe matangazo yao isipokua mgonjwa wa dharura, tujikite kwenye kuwahudumia watanzania fedha Baadae.

"Nimeona habari au tangazo wakisema watawatoa wagonjwa waliopo wodini ndani ya masaa 48 nataka kusema ni marufuku kuondoa wagonjwa waliopo wodini kwasababu kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya madakatari".

"Jambo la Mwisho nazielekeza Hospitali zote za Serikali kujiandaa na kuweka utaratibu mzuri wa kupokea wagonjwa wengi zaidi watakaoshindwa kupata huduma kwenye Vituo binafsi na kuwahudumia hasa kipindi hichi"