Fireboy (28) amefanya mahojiano na Billboard na kuweka wazi kuwa ni Madonna mwenyewe ndiye aliyemtafuta kwa mara ya kwanza na kumchana kuwa yeye ni shabiki wa muziki wake.
"Alinitumia DM kwenye Instagram na kuniambia kuwa alikuwa shabiki, na kwamba alipenda sana wimbo ambao sikuweza kuujumuisha kwenye albamu yangu ya kwanza," alisema Fireboy.
Mnamo Februari 2022, mitandao mbalimbali ilichapisha picha za Fireboy akiwa na Madonna, wote wawili wamevalia mavazi ya rangi nyeusi. Mwezi uliofuatia, walishirikiana katika Remix ya wimbo wa zamani wa Madonna, unaitwa Frozen.