'Nilizaliwa na selimundu, nimeishi nayo maisha yangu yote. Kama mimi nimeweza hata ninyi mnaweza. Nimepambana nayo hadi kuwa staa, nafanya shows mahali popote duniani hata isiwavunje moyo' amesema Adekunle.
Mnano Julai 2022, kwa mara ya kwanza Adenkule alifichua kuwa amekuwa akiishi na ugonjwa wa selimundu tangu kuzaliwa kwake na namna ambavyo alipitia kipindi kigumu katika kupambana na hali hiyo.
Kwa mujibu wa wataalamu Seli Mundu (Sickle Cell) ni ugonjwa ambao hushambulia seli nyekundu za damu pamoja na haemoglobin ambapo huhusisha mtu kuishiwa damu.