Mnamo Oktoba 2023 Lupita kupitia mtandao wake wa Instagram, alifichua kuwa yeye na aliyekuwa mpenzi wake tangu mwaka 2016, Selema Masekela wameachana.
Akifanyiwa mahojiano na Jarida la NET-A-PORTER, Lupita amefunguka sababu kubwa iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano hayo ni manyanyaso na kuumizwa kila mara katika penzi hilo.
"Nilikuwa nikiishi kwa huzuni na uchungu, niliangalia nguvu ya mitandao yangu ya kijamii nikagundua sina haja ya kujifanya mambo yapo sawa ndani wakati kiuhalisia sio kweli, sikutaka kuwa muongo" – Lupita.