
Mfanyabiashara aliyekamatwa
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara za mijini TARURA, msafara huo wa Mkuu wa Mkoa ukipita katikati ya mji wa Manyoni lilionekana gari lililobeba shehena ya sukari, na baada ya kuulizwa walidai wamenunua kwenye duka la mfanyabiashara huyo aliyejulikana kwa jina la Mayengela Mboji.
Baada ya maelezo ya wateja hao Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba aliyeambatana na kamati ya Usalama Wilaya ya Manyoni, wakaingia katika duka hilo na kukagua risiti za mauzo ambapo ikabainika anauzia wateja kwa bei kati ya shilingi 184,000 hadi 189,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50.