Picha ya Ramadhani Brothers
Kundi hilo linaloundwa na ndugu wawili (Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu) wametangazwa washindi kwa umahiri wao katika sarakasi (Acrobatics) usiku wa jana Jumatatu na kuondoka na kibunda cha zaidi ya Tsh Milioni 600.
“Hatimaye safari yetu imefikia hapa, tuna furaha kuwa washindi wa AGT Fantasy League duniani, asante kwa mashabiki wote na washiriki wenzetu” - wameandika Ramadhani Brothers baada ya ushindi huo.