
KIpigo dhidi ya Bochum kinakuwa cha tatu mfululizo baada ya kupoteza michezo miwili iliyopita dhidi ya Lazio wa Ligi ya mabingwa ulaya kwa bao 1-0 na ule dhidi ya Bayer Leverkusen ambao walifungwa 3-0.
Kwa matokeo haya The Bavarian wameachwa alama 8 na Bayer Leverkusen wanaoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga ambao wana alama 58, Bayern Munich wana alama 50 kwenye michezo 22 wapo nafasi ya pili.
Bayern ambao ni mabingwa kwa misimu 11 ya Ligi Kuu Ujerumani huwenda wakamaliza msimu bila kikombe kwani walifungwa kwenye mchezo wa fainali wa German Super Cup mwanzoni mwa msimu pia walitolewa raundi ya 2 kwenye kombe la Ujerumani (German Cup).