Thursday , 15th Feb , 2024

Watendaji  mkoani Simiyu wametakiwa  kutumia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  kwenye mipango yote inayofanyika na itakayofanyika mkoani hapo ili kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa kuzingatia idadi yao na miundombinu iliyopo.

Hayo yamesemwa kamisaa wa sensa ya watu na makazi 2022 Anne Makinda  kwenye  mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 mbele ya  sekretarieti ya mkoa,kamati ya sensa ya mkoa na kamati ya ulinzi  na usalama ya mkoa.

Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema matokeo hayo yatasaidia mkoa huo kupanga mipango ya muda mrefu na mfupi na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 mkoa wa Simiyu umetajwa kuwa wa kwanza wanawake kuongoza kaya na  ndio mkoa wenye idadi kubwa ya watoto huku wilaya ya Itilima ikitajwa kuongoza.