Sunday , 4th Feb , 2024

Nangolo Mbumba ameapishwa kuwa Rais wa nne wa Namibia kufuatia kifo cha Rais Hage Geingob aliyefariki dunia mapema asubuhi ya leo Februari 4, 2024.

Nangolo Mbumba, Rais Mpya wa Namibia

Mbumba aliyekuwa Makamu wa Rais, ameapishwa kuwa Rais wa Namibia na Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Namibia na atakuwa Rais hadi pale Uchaguzi Mkuu utakapofanyika baadaye mwaka huu.

Katika hali ya utulivu baada ya hafla hiyo, Mbumba alitoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa mbunifu mkuu wa katiba na usanifu wa utawala bora wa Namibia.