Saturday , 20th Jan , 2024

Moto umeteketeza bweni moja katika shule ya bweni katikati mwa China na kuwaua wanafunzi 13, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

 

Mwanafunzi mmoja alijeruhiwa katika moto huo katika shule ya Yingcai katika kijiji cha Yanshanpu, shirika la habari la Xinhua liliripoti Jumamosi.

Waathiriwa walitambuliwa kama wanafunzi wa shule ya msingi ya darasa la tatu. Mwalimu mmoja aliliambia gazeti la serikali la Hebei Daily kwamba wote walikuwa wa darasa moja la watoto wa miaka tisa na 10.

Kikosi cha zima moto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao uliripotiwa saa 11 jioni  siku ya Ijumaa na mkuu wa shule hiyo alikamatwa wakati mamlaka zikichunguza chanzo hicho.

Mtu aliyenusurika alikuwa akitibiwa hospitalini na kuripotiwa kuwa "katika hali nzuri", kwa mujibu wa Xinhua.