Saturday , 20th Jan , 2024

Mkali wa Singeli Dulla Makabila amefunguka kupokea vitisho kupitia ujumbe wa Instagram (DM) kutoka kwa Haji Manara baada ya kuachia wimbo wake mpya wa Furahi.

Picha ya Haji Manara na Zaylissa kushoto ni Dulla Makabila

Dulla Makabila amevujisha message hizo za Haji Manara zinazosema

“Umeanza mimi nakuja kumaliza, hii video yako ya kujiliza itakuwa gumzo na usije kunilaumu Ninazo msg zako zote. Kaa ukijua umechokoza gwiji wa hizi kazi usije baadaye kutafuta huruma”.

“Umemtukana na kutaka kumdhalilisha mtu mwenye silaha zako kibao na akakuhifadhi siku zote. Sasa kwakuwa unataka kiki na trending utaipata hasa. Usiku mwema na jiandae kisaikolojia”.

Siku 2 zilizopota Haji Manara alivalisha pete ya uchumba mke wa zamani wa Dulla Makabila Zaylissa.