Sunday , 31st Dec , 2023

Tume Huru ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, imemtangaza Félix Tshisekedi, kuwa ndiyo mshindi wa uchaguzi katika kiti cha Urais kwa asilimia 73% akimshinda mpinzani wake wa karibu Moise Katumbi ambaye amepata asilimia 18% ya kura.

Félix Tshisekedi

Uchaguzi wa Desemba 20, 2023, wa DRC ulikumbwa na changamoto nyingi huku wagombea kadhaa wa upinzani walikuwa wakitaka yafanyike marudio ya uchaguzi huo.

Takribani theluthi mbili ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa, wakati asilimia 30 ya mashine za kupigia kura hazikufanya kazi siku ya kwanza ya upigaji kura, kwa mujibu wa waangalizi wa uchaguzi.

Tshisekedi alikuwa akichuana na wapinzani wake kina Moise Katumbi, Martin Fayulu na Denis Mukwege katika uchaguzi ulioghubikwa na malalamiko ya wapinzani hao.