
mbunge wa jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul
Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 27, 2023, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Babati, Victor Kimario na kusema ameifuta baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa kupitia kwa wakili Peter Madeleka chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Ambapo kwa upande wake Wakili Madeleka amesema hawajakubaliana na maamuzi hayo na kwamba watakata rufaa.
Kesi hiyo dhidi ya Mbunge Paulina Gekul ilifunguliwa na wakili huyo kwa kushirikiana na wenzake wakidai alimfanyia kitendo cha ukatili kijana huyo kwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.