
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga akizungumza na #SupaBreakfast ya #EastAfricaRadio amesema zoezi la kutafuta miili mingine linaendelea huku akisema taarifa zaidi zitaendelea kutolewa
"Kwakweli mpaka sahivi na sisi hatuna uhakika ambacho tunachojua tumepata mvua, ambayo imeporomosha mawe na matope mazito kutoka mlimani, lakini serikali imeleta watafiti wa madini wameingia hapa jana jioni na sasa hivi navyoongea na ninyi wameshaanza kupanda kuelekea juu mlimani kuangalia lile tope ni tope la kawaida la mvua au kulikuwa na kitu kingine nadhani baada ya hapo tutajulishwa"
"Tunachokifanya ni kutafuta miili kwenye matope kwasababu jana kwa kufanya hivo tulifanikiwa kupata miili ya watu mbalimbali na tunafanya hivo kwa kubahatisha kwasababu zipo familia ambazo zimeripoti kutowaona baadhi ya ndugu zao hivo tunaamini kwa kutafuta kwenye matope tunaweza kuwapata"