Saturday , 2nd Dec , 2023

Disemba 1 ni siku ya UKIMWI duniani, msanii Ferooz aliwahi kutoa wimbo wake wa Starehe ambao unazungumzia alivyopata Ugonjwa huo.

Picha ya Ferooz

Hapa anafunguka anayokutana nayo baada ya kuachia wimbo ule

 

"Kuna mazingira nilikutana nayo na bado nakutana nayo mpaka le. Unaweza ukakutana na mtu akashtuka na kukwambia wewe si ulishafariki kwa sababu aliona kwenye video, mwingine anakupa pole au kukunyanyapaa anajua kama umeathirika".

 

"Wapo wanaoamini kwamba nimeathirika na kupata HIV. Wakati mwingine unaweza ukapungua kutokana na sababu za maisha lakini watu wakikuona wanajua ndio tayari kwa kuzingatia niliimba ule wimbo" amesema Ferooz 

 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.