Friday , 1st Dec , 2023

Mwanamuziki Vanessa Mdee ametusanua kuwa moja ya uamuzi wake bora aliowahi kuufanya ni kuacha kutumia vinywaji venye vilevi ‘Alcoholic’.

Picha ya Vanessa Mdee

Mama huyo wa watoto wawili anayeishi na mchumba wake Rotimi nchini Marekani ameshea hilo kupitia ‘Insta Story’ yake inayoeleza kwamba inakaribia miaka minne sasa bila kutumia kilevi chochote.

“Sijapata kinywaji chenye kileo kwa takriban miaka minne. Moja ya uamuzi bora kabisa ambao nimewahi kuufanya. Asante mungu kwa neema hii” ujumbe wa Vanessa Mdee

Upi uamuzi wako bora ambo unajivunia kuufanya mpaka sasa?