Friday , 1st Dec , 2023

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza nyumba moja katika eneo la barabara ya Makupa mtaa wa Mlalakuwa kata ya Makongo jijini Dar es Salaam

Katika moto huo uliotokea asubuhi la leo Desemba 1/2023 watu watano wamenusurika kifo akiwemo mtoto aliyekuwa anajiandaa kwenda shule

Akiongea na EATV mmiliki wa nyumba hiyo Gabriel Makupa anasema moto ulianza kwenye chumba cha dada wa kazi na baadae ukaenea nyumba nzima na walijitahidi kuumiza lakini hawakufanikiwa mpaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilivyofika.

Akielezea mali zilizoungua anasema hakuna kitu chochote walichofanikiwa kuokoa isipokuwa watu wote waliopo ndani walitoka salama.

Mali zilizoteketea ni pamoja na Camera za picha zaidi ya nane, vifaa vyote vya ndani na moja ya gari imeungua kidogo