
Kiwanja cha ndege Kigoma kinachofanyiwa ukarabati
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya ndege nchini (TAA) kwa kukagua upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma, mkoani Kigoma
Kihenzile amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inachukulia sekta ya uchukuzi kwa njia ya anga kama mishipa ya ukuzaji uchumi na shughuli mbalimbali za utoaji huduma kwa wananchi ndani na nje ya nchi, ndiyo maana imewekeza fedha nyingi kwenye maboresho,ukarabati na upanuzi wa viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege kwa ujumla.
Kihenzile amesema kuwa serikali inajenga miundombinu ya viwanja vya ndege nchini ili kulifanya Taifa la Tanzania kuwa kubwa na lenye nguvu ya ushawishi kiuchumi kikanda na kimataifa.
Upanuzi wa uwanja huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege kutoka mita 1800 hadi 3000, eneo la megesho ya ndege , mnara wa kuongozea na jengo la abiria huku ukitarajiwa kuhudumia abiria laki nne kwa mwaka na kuwekewa taa za kuongozea ndege ili utumike kwa saa 24 huku ukipokea ndege kubwa zaidi