Tuesday , 28th Nov , 2023

Ndege ya kampuni ya Unity Air 5H-MJH aina ya EMBRAER 120 iliyokuwa na watalii 30, marubani 2 na mhudumu mmoja imepata ajali asubuhi ya hii leo Novemba 28, 2023, iliyotokana na tatizo la kiufundi wakati ikitua katika kiwanja cha ndege cha Kikoboga kilichopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi

Ndege iliyopata ajali

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANAPA imesema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea Zanzibar, ambapo kutokana na juhudi zilizofanywa na marubani wa ndege hiyo pamoja na maafisa wa kiwanja hicho na walihakikisha hakuna madhara yanayotokea ambapo watu wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo walitoka salama na kuendelea na shughuli zao za utalii

Aidha TANAPA imekwishawasiliana na idara ya uchunguzi wa ajali za ndege iliyopo Wizara ya Uchukuzi kwa ajili ya taratibu zingine na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.