Thursday , 23rd Nov , 2023

Tukiwa tunaelekea kwenye wiki ya 13 ya Ligi Kuu soka Uingereza EPL, EA Radio Fantasy League tunakuletea orodha ya wachezaji ghali zaidi kwenye soka la wachezaji la Premier League Fantasy League (PFL).

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland ndio mchezaji anayeuzwa kwa fedha nyingi zaidi unaweza kumnunu kwa pauni milioni 14. Na ndio mchezaji anayeongoza kwa kukusanya alama nyingi zaidi ana alama 96.

Nafasi ya pili yupo Mohamed Salah wa Liverpool anauzwa kwa pauni milioni 13. Nafasi ya tatu anakamata kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kelvin De Bryune ana uzwa kwa pauni milioni 10.2. 
Son Heung-min wa Tottenham thamani yake sokoni kwenye soko la Fantasy ni pauni milioni 9.7 anashika nafasi ya 4 kwenye orodha ya ghali zaidi. Nafasi ya 5 anakamata wing awa Arsenal Bukaya soka anapatikana kwa dau la pauni milioni 8.6.

Unaweza kusajili wachezaji hawa ili uijiongeze nafasi ya kuwa mshindi wa kila mwezi wa EA Radio Fantasy League ambayo inadhaminiwa na DSTV Tanzania na Vodacom Tanzania.